Biashara yako inaweza kukua bila wewe, kupitia mfumo wa biasharatovuti ya biasharaaplikesheni ya simumtandao wa intaneti

Tunageuza changamoto zako za kiutendaji kuwa hatua za haraka na zinazo suluhishwa, kupitia mifumo inayojiendesha yenyewe.

Hesabu
100%Udhibiti wa Fedha na Ripoti
Muda Wote
24/7Amani ya Akili na Muda
Malipo
Papo HapoMalipo kwa Njia ya Mtandao
Taarifa
SalamaTaarifa Zinahifadhiwa
Ufanisi
OtomatikiMfumo Unajiendesha Wenyewe
Usalama
100%Kuondoa Makosa na Wizi

Jinsi Tunavyofanya Kazi

Kutoka Wazo Hadi Uzinduzi

Kila mradi unapitia hatua nne zilizopangwa vizuri, ili matokeo yawe sahihi, thabiti na yanayoendana na uhalisia wa biashara yako.

01

Wazo

Tunakusikiliza kwa makini, tunaelewa lengo la biashara yako, na tunaandaa mpango kazi wenye uwazi wa kile kitakachojengwa.

02

Muundo

Tunabuni muundo na muonekano wa suluhisho lako kabla ya ujenzi kuanza, ili uweze kuona na kuidhinisha mwelekeo mapema.

03

Ujenzi

Timu yetu inajenga na kupima suluhisho hatua kwa hatua, tukikupa taarifa kila mara mradi unavyoendelea.

04

Uzinduzi

Tunazindua, tunafundisha timu yako kutumia mfumo, na tunabaki karibu kwa msaada na uboreshaji unapohitajika.

Uwazi kamili katika kila hatua, hakuna cha kukupa mshangao, hakuna maswali yasiyojibiwa.

Uwezo Wetu

Haya Ndiyo Tunayoyajenga

Kila biashara ni ya kipekee, na kila suluhisho tunalolijenga huundwa mahususi kwa ajili yake. Hii si historia ya miradi ila ni uthibitisho wa tunachokijua kufanya vizuri.

01

Mifumo ya Uendeshaji wa Biashara

Mifumo ya kusimamia biashara, mauzo na taarifa za wateja, ulioundwa kufuata mtiririko wa kazi wa shirika lako.

  • Mfumo hai wa data
  • Ripoti za wakati halisi
02

Majukwaa ya Simu na Wavuti

Programu za simu na tovuti zenye uwezo wa matumizi kamili, kutoka usajili wa mtumiaji hadi malipo ya mtandaoni.

  • iOS na Android
  • Muunganiko wa malipo
03

Tovuti za Biashara na Taasisi

Tovuti za kifahari zenye muundo unaoendana na chapa yako, kasi ya hali ya juu, na msingi thabiti wa SEO.

  • Muundo wa kipekee
  • Uwekaji mtandaoni thabiti
04

Chapa na Vifaa vya Masoko

Nembo, vitambulisho vya chapa na vifaa vya masoko vinavyowasilisha ujumbe wako kwa usahihi.

  • Vitambulisho vya chapa
  • Vifaa vya kuchapisha na kidijitali

Wanachosema Wateja

Tunaaminiwa na Biashara, Mashirika na Taasisi

Kutoka Kigoma hadi Mbeya, na kila mahali katikati, hawa ni baadhi ya wamiliki wa biashara na taasisi tunaowahudumia kila siku. Hii ndiyo sababu wanaendelea kuchagua DataSoft.

Tangu DataSoft wanijengee mfumo wa duka langu, nimeacha kuandika mauzo kwa mkono. Sasa naona kila kitu, bidhaa zilizouzwa, faida ya siku, kwa dakika moja tu. Kazi nzuri ya kweli!

Godwin Marko ShauriMfanyabiashara · Kasulu, Kigoma

Mtandao wetu wa shule sasa unafanya kazi bila kukwama, na walimu wanatumia mfumo mmoja kuweka alama za wanafunzi. Timu ya DataSoft ilituelewa kwa haraka na kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa.

Neema IsayaMkurugenzi, Shule ya Awali Tumaini · Mwanza

Tovuti mpya ya hoteli yetu inapokea wageni kutoka nje ya nchi kila wiki. Ni ya haraka, nzuri kuangalia, na haijawahi kuzimika hata siku moja tangu izinduliwe.

Hamisi Ally JumaMeneja, Hoteli ya Baobab · Dodoma

Nembo na vifaa vya chapa walivyonitengenezea DataSoft vimenipa taswira ya kitaalamu ambayo wateja wanaiona mara moja. Naona tofauti kubwa katika mauzo yangu ya mtandaoni.

Grace MremaMwanzilishi, Chic Boutique · Arusha

Mfumo wa kusimamia hisa na wasambazaji umetuokoa saa nyingi kila wiki. Kila idara sasa inaona taarifa zile zile, wakati ule ule. Hii ndiyo tija tuliyoihitaji.

Elias MushiMkurugenzi Mtendaji, Mbeya Fresh Produce Ltd · Mbeya

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Una Swali? Tuko Hapa

Majibu ya haraka kwa mambo ambayo wateja wetu huuliza mara kwa mara kabla ya kuanza mradi.

Tunarahisisha utendaji wa kazi zako kwa mifumo ya kisasa inayojiendesha yenyewe kupitia ● Ukuzaji wa Programu Maalumu kwa mifumo thabiti na programu za simu ● Ubunifu wa Tovuti na Uhifadhi wa tovuti ● Usanifu wa Mitandao ya Ofisini kwa miundombinu salama na yenye kasi ● Ubunifu wa Michoro ya Chapa kwa muonekano wa kitaalamu na wenye mguso wa kihisia. Unaweza kuchagua huduma moja au kuziunganisha zote nne kuwa mradi mmoja.

Inategemea ukubwa wa mradi, lakini tunaweza kuanza kukujengea mfano wa kwanza (prototype) ndani ya masaa 48 baada ya mazungumzo yetu ya kwanza. Kila mradi hupitia hatua nne, Wazo, Muundo, Ujenzi na Uzinduzi. Tutakupa muda kamili baada ya kuelewa mahitaji yako.

Kila mradi ni wa kipekee, hivyo bei hutegemea ukubwa na mahitaji yake. Fomu yetu ya mawasiliano hukuuliza wigo wa bajeti yako ili tuweze kukushauri kifurushi kinachokufaa. Ushauri wa kwanza ni bure kabisa.

Ndiyo, tunafanya kazi popote ulipo. Nyumbani kwetu ni Mwanza, lakini huduma zetu zinafika kote Tanzania, kutoka Kigoma na Arusha, hadi Dodoma na Mbeya, kupitia mawasiliano ya mtandaoni na simu, na tunasafiri panapohitajika kwa miradi ya mitandao ya ofisini.

Kabisa. Wakati wa kujaza fomu ya mawasiliano unaweza kutuambia kama huna muundo bado, na timu yetu itakushauri na kukubunia chaguo kutoka mwanzo. Hauhitaji kuja na kila kitu tayari.

Ndiyo. Kila mradi tunaoujenga unakuja na msaada endelevu, ufuatiliaji wa upatikanaji (uptime), na nakala za akiba za mara kwa mara. Timu yetu inabaki karibu nawe, popote ulipo, kwa msaada wowote unaohitajika baada ya uzinduzi.

Ndiyo. Miradi yetu yanajumuisha vyeti vya usalama (SSL), ulinzi dhidi ya matatizo ya kawaida ya mtandao, na nakala za akiba za taarifa zako, ili biashara yako ibaki salama na ifanye kazi bila wasiwasi.

Jaza fomu yetu fupi ya mawasiliano hapo chini, tupigie simu, au tutumie ujumbe wakati wowote unaokufaa, tuko tayari kukusikiliza. Kuweka miadi hutupatia nafasi bora zaidi ya kukuhudumia, lakini hupaswi kusubiri hadi upate moja ili kuwasiliana nasi. Maswali machache tu yanatosha kutusaidia kuelewa mradi wako, na timu yetu itawasiliana nawe ndani ya saa chache kuanza mazungumzo, bila malipo.

Wasiliana Nasi

Tuambie Kuhusu Mradi Wako

Majibu machache tu yanatusaidia kukupa ushauri sahihi mara ya kwanza. Hii si fomu ya kawaida, ni mwanzo wa mradi wako.

Ushauri wa Kwanza, BureMfano wa Kwanza (Prototype) Ndani ya Masaa 48Msaada Baada ya UzinduziUsalama Kamili kwenye utendaji wa mfumo
Wazo Bora + Timu Bora + Mfumo Bunifu = Ushindi Wako
Hatua 1 kati ya 6

Mradi wako ni mpya au unaboresha uliopo?

Hii hutusaidia kujua tuanzie wapi, kutoka mwanzo kabisa au kuboresha kilichopo.